NAIROBI:Waziri wa Afya aachiliwa na polisi
3 Agosti 2007Waziri wa Afya nchini Kenya Bi Charity Ngilu anasisitiza kuwa hajavunja sheria yoyote.Bi Ngilu alikamatwa na polisi jana jioni baada ya kumsaidia mwanaharakati mmoja kutoka kwenye kituo cha polisi alikokuwa anazuiliwa kwa madai kwamba alikuwa anamsaidia kupata huduma za daktari.Bi Ngilu alikamatwa alipokuwa akimpeleka mwanaharakati huyo hospitali na kuzuiliwa kwenye makao makuu ya Uchunguzi wa Uhalifu mjini Nairobi.Polisi wanakataa kutoa maelezo yoyote kuhusu hatu hiyo ila kuthibitisha kuwa sheria sharti zifuatwe ....hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Polisi Eric Kiraithe.Wakili wa waziri huyo wa Afya Bwana Paul Muite anashikilia kuwa Bi Ann Njogu aliyekamatwa alipigwa vibaya na polisi na alihitaji matibabu ndipo Bi Ngilu akaingilia kati.Bi Njogu alitibiwa na kutoka hospitali kasha kurudi polisi.Kulingana na Bwana Muite hakutoroka.