Nakala ya kinasa sauti za marudani iliyoanguka yakamilishwa
4 Januari 2025Mkanda huo wa sauti huenda ukawa na majibu ya kilichotokea dakika za mwisho kwenye ndege ya Shirika la Jeju Air, iliyokuwa imewabeba abiria 181 na wahudumu kutoka Thailand kwenda Korea Kusini Jumapili iliyopita, wakati ilipotua kwa kasi na kugonga ukuta wa uwanja ndege na kulipuka.
Wizara ya ardhi ya Korea Kusini imesema kazi ya kukusanya data kutoka kwa kinasa sauti hicho itakamilishwa leo, na kisanduku cha kunasa data za safari kinaendelea kutayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa hadi Marekani kwa ajili ya uchunguzi. Wachunguzi wa Korea Kusini na Marekani, ikiwa ni pamoja na wale kutoka kampuni iliyotengeneza ndege hiyo ya Boeing, wamekuwa wakipekuapekua eneo la mkasa katika mji wa kusini magharibi wa Muan tangu mkasa huo ulipotokea ili kubainisha chanzo cha ajali hiyo.