1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Namibia yamchagua rais wa kwanza mwanamke

4 Desemba 2024

Namibia imemchagua rais wa kwanza mwanamke baada ya chama tawala cha SWAPO kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.

Namibia Windhuk 2024 | Präsident Mbumba begrüßt SWAPO-Kandidatin Nandi-Ndaitwah
Rais wa Namibia Nangolo Mbumba akisalimiana na Rais Mteule Netumbo Nandi-Ndaitwah wa chama tawala cha Namibia cha SWAPO, kwenye mkutano wa kabla ya uchaguzi wa Namibia, Novemba 24, 2024.Picha: Noah Tjijenda/REUTERS

Tume ya Uchaguzi ya Namibia ECN, imemtangaza Makamu wa Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah, kushinda kwa zaidi ya asilimia 57 ya kura akifuatiwa na mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha Patriots for Change IPC, Panduleni Itula aliyepata asilimia 25.5. Itula na chama chake cha IPC lakini wamesema hawatambui matokeo ya uchaguzi huo ambao wanadai ulikumbwa na udanganyifu mkubwa. Nandi-Ndaitwah mwenye miaka 72, anakuwa mwanamke wa kwanza kuitawala nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, iliyoongozwa na chama cha SWAPO tangu ilipopata uhuru mwaka 1990.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW