1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamibia wanamchagua rais wao katika uchaguzi wa leo

27 Novemba 2024

Makamu wa rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah ni miongoni mwa wapiga kura wa kwanza katika uchaguzi wa leo ambao huenda ukamfanya kuwa rais wa kwanza mwanamke wa taifa hilo.

Namibia | Wahlen
Makamu wa Rais wa Namibia na mgombea urais wa SWAPO Netumbo Nandi-Ndaitwah wakati wa kupiga kura katika uchaguzi wa Windhoek, Namibia, Novemba 27, 2024.Picha: Noah Tjijenda/REUTERS

Hiyo ni wakati chama chake cha SWAPO kikikabiliwa na ushindani mkali unaotishia udhibiti wake wa miaka 34 madarakani. Nandi-Ndaitwah mwenye umri wa miaka 72, wa chama cha South West Africa People's Organization alipiga kura yake katika mji mkuu Windhoek na kuwatolea wito wapiga kura milioni 1.5 waliosajiliwa wajitokeze kwa wingi vituoni. Chama cha SWAPO kimeitawala nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini tangu uhuru mwaka 1990 lakini, huku kukiwa na malalamiko kuhusu ukosefu mkubwa wa ajira na ukosefu wa usawa, Nandi-Ndaitwah anaweza kulazimishwa kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi kama atashindwa kupata angalau nusu ya kura. Ana wapinzani wanne wakuu akiwemo Panduleni Itula, mwenye umri wa miaka 67, ambaye ni daktari wa zamani wa meno na mwanasheria aliyeanzisha chama cha Independent Patriots for Change mwaka wa 2020. Itula alipata asilimia 29 ya kura katika uchaguzi wa 2019, aliposhindwa na kiongozi wa SWAPOHage Geingob, aliyepata asilimia 56 ya kura.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW