1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani kuongoza Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya?

7 Juni 2024

Nani atakayepata nafasi ya kuiongoza Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya katika kinyan'ganyiro cha kuwania nafasi hiyo? Ursula von der Leyen anatetea nafasi yake lakini je kuna mgombea mwengine?

Uchaguzi Bunge la Ulaya 2024
Bando la uchazizi wa Ulaya likiwa kwenye moja ya jengo Ujerumani.Picha: Ardan Fuessmann/IMAGO

Wakati raia wa Ulaya wakiendelea na mchakato wa kuchagua bunge jipya la Umoja wa Ulaya, wanasiasa wa bara hilo wanajiuliza iwapo rais wa sasa wa Halmashauri Kuu ya Umoja huo, ataendelea kushikilia nafasi yake na kama hatofanikiwa kufanya hivyo basi nani atakayechukua nafasi hiyo?

Yoyote anayetaka kazi hiyo, kwanza ni lazima avuuke vizingiti hivi viwili, kwanza ni lazima ateuliwe na viongozi wa Ulaya katika mazungumzo ya faragha baada ya uchaguzi wa bunge na pili atakayeteuliwa ni lazima athibitishwe na wengi katika bunge la Ulaya. 

Mwaka 2019, Ursula von der Leyen aliponea chupuchupu katika kizingiti hicho cha pili cha kuidhinishwa bungeni kwa tofauti ya kura tisa tu. Kwa hiyo sio rahisi kufikiria kuwa bunge hili la mwaka 2024 litakuwa rafiki kwake.

Soma pia:Ireland na Jamhuri ya Czech zapiga kura katika uchaguzi wa bunge la EU

Licha ya hayo, bado von der Leyen ni mtu aliye katika nafasi ya juu ya kuchukua tena nafasi hiyo ya kuiongoza Halmashauri Kuu ya Ulaya. Ana matumaini kuwa namna alivyoshughulikia janga la UVIKO-19 na vita vya Urusi na Ukraine vitampa angalau nafasi nzuri ya kuungwa mkono. 

Hata hivyo, mtindo wake wa kuendesha mambo kivyake umekosolewa na makamishna wenzake.

Pia tabia yake ya kutozungumza na vyombo vya habari inajulikana wazi na anaonekana kama kiongozi mwenye ukosefu wa uwazi.

Kipimo cha ufanisi wake

Wakati alipokuwa na makubaliano makubwa na kampuni ya Pfizer ya kutengeneza chanjo ya UVIKO-19 mwaka 2021, maelezo ya mkataba huo hayajawahi kuwekwa hadharani hadi sasa.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der LeyenPicha: Jakub Porzycki/NurPhoto/picture alliance

Kamisheni yake ilikataa kutoa maelezo hayo, ikiombwa kufanya hivyo kwa kuzingatia uhuru wa habarii au hata kutoa maelezo ya jumbe zilizotumwa kati ya Ursula vo der Leyen na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Pfizer, Albert Bourla.

Soma pia:Uchaguzi wa bunge la Ulaya waanza Uholanzi

Kukataa huko sasa ni sehemu ya gumzo la gazeti la The New York Times kufungua kesi dhidi ya kamisheni hiyo. 

Von der Leyen, raia wa Ujerumani anayetokea katika kundi la vyama vya siasa za wastani za mrengo wa kulia, EPP, alipata nafasi ya kuiongoza Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya mwaka 2019 kwa msaada wa kura za waliberali na wanademokrasia wa kisoshalisti.

Wengine waliojitosa kwenye kinyang'anyiro

Kando na hilo ukizungumzia mtu mwengine anayeonekana kuchukua nafasi hiyo jina la Mario Draghi mwanasiasa kutoka Italia haliwezi kukosa kutajwa. Baadhi wanaamini anaweza kuchukua nafasi ya von der Leyen.

Raia wa Ulaya wakipiga kurakuchagua wawakilishi wao wa UlayaPicha: Ramon van Flymen/EPA

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Italia,  na rais wa benki kuu ya Ulaya amekuwa nje ya masuala ya uongozi tangu serikali yake iliposambaratika mwaka 2022. 

Draghi amekuwa akifanya kazi ya kuangalia ripoti za Umoja huo kujaribu kuuinua uchumi wake unaojivuta ukiwa nyuma ya Marekani.

Uchumi wa Umoja wa Ulaya umeyumba kufuatia janga la UVIKO-19 na kupanda kwa gharama za nishati ya umeme kufuatia vita vya Urusi na Ukraine. 

Soma pia:Utafiti: Wajerumani wachache kujitokeza uchaguzi wa Ulaya

Vyombo vya habari vya Italia vimeripoti kwamba rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, aliyemuunga mkono Leyern mwaka 2019, anaonekana safari hii kutupa karata yake kwa Mario Draghi. Italia na Ufaransa wanashirikiana katika masuala mengi ya kisera. 

Hata hivyo, ukweli wa mambo utajulikana pale viongozi wa Umoja wa Ulaya watakapoanza mchakato wa kumteua rais wa Halmashauri Kuu na jina lolote litakaloungwa mkono ndilo litakaloibuka na kuanza mchakato mwengine wa kuidhinishwa bungeni kama ilivyokuwa kwa von der Leyen mwaka 2019.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW