Nani mchezaji bora barani Ulaya?
15 Agosti 2014Shirikisho la Kandanda Ulaya – UEFA limewataja wachezaji hao watatu baada ya orodha ya wagombea 10 kupunguzwa kupitia kura zilizopigwa na waandishi wa habari kutoka mashirikisho 54 wanachama wa UEFA.
Neuer ndiye mlinda lango kwa kwanza kuwahi kujumuishwa katika orodha ya mwisho ya wagombea katika mfumo wake wa sasa. Alichaguliwa kama Mchezaji Bora wa Kandanda nchini Ujerumani mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya kuisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Dunia nchini Brazil na pia klabu yake ya Bayern Munich kunyakua mataji mawili msimu uliopita.
UEFA imesema Neuer alionekana sana katika Kombe la Dunia huku akifanya maajabu katika lango Die Mannschaft. CR7 wa Ureno alikuwa miongoni mwa walioshindwa kumfunga NEUER katika dimba hilo la Brazil, lakini akamfunga katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ambapo Real Madrid waliibuka washindi wakati akifunga magoli 17 katika dimba hilo.
Real Pia wameshinda Kombe la Super Cup Uhispania msimu wa 2013-2014. Robben aliisaidia Uholanzi kumaliza katika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia na akashinda taji la Bundesliga na Kombe la Shirikisho la Soka Ujerumani – DFB akiwa na Bayern.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Yusuf Saumu