1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyama vya siasa Ujerumani

9 Juni 2017

Uchaguzi mara hii Ujerumani unaweza kuwa mgumu kuliko Kansela wa Ujerumani alivyotarajia. Hapa utaweza kuwatambua nani ni nani katika siasa za Ujerumani.

Saarland Landtagswahlen Wahlplakate SPD  CDU
Bango la Uchaguzi wa 2017 UjerumaniPicha: Getty Images/S. Gallup

Ujerumani inajitayarisha na uchaguzi ambao utafanyika tarehe 24.09.2017.

Tuanze na chama cha Christian Democratic Union ( CDU ) /  Christian Social Union/ CSU

Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: Reuters/A. Marcarian

Rangi: Nyeusi

Kiongozi: Angela Merkel

Wanachama: 430,000

Wapigakura: Wengi wanaumri uliozidi miaka 60, wanachama wengi bado ni wafuata dini na wanakwenda kanisani, ni wale wanaoishi nje ya mji hasa katika maeneo ya kusini mwa Ujerumani. Chama cha CDU kimefanya vizuri pia kwa wafanya biashara wadogowadogo na watu wenye elimu ya chini au ya kati.

Matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2013: Asilimia 41.5  Viti: 311/630

Historia: CDU kiliundwa mwaka 1950 magharibi ya Ujerumani baada ya. Vita Vya Pili vya dunia. Kilikuwa ni chama tawala  baada ya vita katika sehemu yamagharibi ya Ujerumani na baadae chama hicho kiliunganisha Ujerumani na kuongoza serikali kwa muda wa miaka 47 kati ya 67, kikishirikiana na chama ndugu cha Christian Social Union ( CSU )

Kansela wa mwanzo alietokea chama hicho ni Kansela Konrad Adenauer ambaye aliongoza kuanzia mwaka 1949 hadi 1963 ambaye pia tunaweza kusema ndie muanzilishi wa chama hiki.

Jukwaa: Angela Merkel anaendeleza utamaduni wa chama hicho lakini pia mambo mapya ameyaingiza katika chama cha CDU. Akishirikiana na waziri wa fedha  Wolfgang Schäuble wapiga kura Ujerumani wanaamini ataulinda uchumi wa Ujerumani kuwa salama. Kansela Merkel  anapinga pia ndoa za jinsia moja. Lakini sera zake za wakimbizi zimemsababishia  changamoto.

Mshirika anayependelewa ili kuunda serikali ya muungano: FDP,SPD, na labda chama cha Kijani

SOCIAL DEMOCRATIC PARTY ( SPD )

Kiongozi wa SPD Martin SchultzPicha: Reuters/M. Dalder

Rangi: Nyekundu

Kiongozi: Martin Schultz

Mgombea Ukanela: Martin Schultz

Wanachama: 440,000

Wapigakura: Chama cha SPD tangu hapo awali kinajulikana kuwa chama cha tabaka la wafanya kazi. Chama hiki kina wafuasi wengi katika sehemu za viwanda magharibi mwa Ujerumani hasa katika sehemu ya Ruhr katika sehemu Jimbo la North Rhine- Westphalia, Hesse, na kusini mwa Saxony.

Matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2013: Asilimia 27.7 viti: 193/630

Historia: SPD ni chama cha zamani nchi Ujerumani kilichoundwa mwaka 1875. Mwanzo chama hicho kilikuwa kama mwamvuli wa  mashirika ya vyama vya mrengo wa kushoto, wafanya biashara, na wakomunisti.

Kansela wa mwanzo wa chama hicho ni Willy Brandt ambaye aliongoza Iliyokuwa Ujerumani  magharibi  kuanzia 1969 hadi 1974.

Chama hiki kwa ujumla kimekuwa katika serikali ya Ujerumani kwa miaka 37.

Jukwaa: Nguvu ya chama cha SPD ni sera za jamii ambapo inasimamia kwa nguvu miundombinu ya kijamii. Lakini kutambulishwa kwa mageuzi ya soko la ajira katika 2010 yaliofanywa na  Kansela Gerhard Schröder mwanzo wa 2000  ulikifanya chama hicho kuporomoka katika kuungwa mkono.

Mshirika anayependelewa ili kuunda serikali ya muungano: Wanazingira au chama cha Kijani, CDU, na labda mrengo wa kushoto.

DIE LINKE, MRENGO WA KUSHOTO

Kiongozi wa Die Linke ( Chama cha mlengo wa kushoto ) Katja KippingPicha: picture-alliance/dpa/M. Balk

Rangi: Nyekundu

Viongozi: Katja Kipping, Bernd Riexinger

Wagombea: Sahra Wagenknecht, Dietmar Bartsch

Matokeo ya uchaguzi wa 2013: Asilimia 8.6 viti: 64/630

Wanachama: 60,000

Wapiga kura: Wengi wao ni wale wa maeneo ya zamani ya Mashariki ya Ujerumani ambapo wapiga kura wengi wanakuwa wale wakomunisti wa zamani waliounga mkono serikali ya zamani ya GDR, wakati Ujerumani bado ilikuwa imegawika upande wa Mashariki na Magharibi.

Historia: Japo kuwa chama hicho kiliundwa 2007, chama hiki cha mrengo wa kushoto kina historia ndefu. Kimetokana na chama cha Socialist Unity Party  ( SED ) ambacho kiliongoza Ujerumani ya Mashariki ya GDR.

Jukwaa: Chama  cha  Die Linke ni chama pekee kinachokataa utumiaji wa majeshi nje ya Ujeramanni, na pia kinataka Jumuia ya kujihani ya NATO iondolewe na kinapigania pia kuongezwa kiwango cha chini cha mapato nchini Ujerumani na  kuwa euro 10 kwa saa.

Mshirika anayependelewa ili kuunda serikali ya muungano: SPD, Greens

THE GREEN PARTY ( Bündnis 90/Die Grünen )

Kiongozi wa chama cha Green Cem ÖzdemirPicha: Getty Images/J. MacDougall

Rangi: Kijani

Viongozi: Cem Özdemir, Simone Peter

Wagombea: Cem Özdemir, Katrin Göring Eckardt

Matokeo ya Uchaguzi wa 2013: Asilimia 8.4 Viti: 63/630

Wanachama: 60,000

Wapiga kura: Ni chama kinachotegemea  sana wasomi, na wakaazi wa miji mikubwa katika sehemu ya magharibi ya Ujerumani, hususan miji yenye vyuo vikuu vingi.

Lakini wapiga kura wa chama hiki wamebadilika katika historia yake ya miaka  30. Wapiga kura wa sasa ni chini ya umri wa miaka  35.

Historia: Chama hiki kina mafanikio makubwa katika kuwafikia watu wenye tamaduni mbalimbali. Chama cha Green kilichipuka mwaka 1980 kutokana na maandamano mbalimbali yakiwemo yale ya kupinga  matumizi ya nyuklia hadi upatikanaji wa haki za wanaofanya mapenzi ya watu wa jinsia moja na bila ya shaka kulinda mazingira. mafanikio yao makubwa ni kuweza kuyaingiza mambo yote hayo katika siasa na chama hicho kilianzishwa rasmi mwaka 1993.

Chama cha Green kilitambuliwa zaidi kilipoamua kuwa na ushirikiano  na chama cha Gerhard Schröder cha SPD katika shirikisho la serikali ya muungano.

Jukwaa: Kuna mgawanyiko wa wale wanaoitwa "realos" yaani wanaoingalia hali kwa uhalisia na wale wanaoitwa "fundis" yaani wenye msimamo mkali ndani ya chama hicho cha kijani . "Realos" wameanza kuwa na nguvu zaidi ndani ya chama hicho, kufikia hadi sasa kuwa wana ushirikiano na chama cha wahafidhina cha CDU katika sehemu ya kusini ya jimbo la baden Wüttemberg.

Mshirika anayependelewa ili kuunda serikali ya muungano: SPD

Alternative for Germany ( AfD )

Kiongozi wa chama cha AfD Frauke PetryPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Rangi: Buluu ya bahari

Viongozi: Frauke Petry, Jög Meuthen

Wagombea : tbd

Wanachama: 27,000

Wapigakura: Chama hiki kimechukuwa idadi ya wanachama kidogodogo kutoka kila chama isipokuwa wale wa chama cha Kijani. Kina nguvu kwa watu wenye kipato cha chini kabisa na wasiokuwa na elimu ya juu. Na kati ya wanachama wao asilimia 15 tu ni wanawake.

Matokeo ya uchaguzi ya mwaka 2013: asilimia 4.7 viti: 0/360

Historia: Chama hiki cha siasa kali za  mrengo wa kulia kimeanza miaka minne iliyopita. Kiliundwa miezi mitano kabla ya uchaguzi wa 2013. Chama hicho kilikaribia kuingia katika bunge la Ujerumani.

2016 chama cha AfD kilikuwa chama pekee kilichoridhishwa na hatua ya kuchaguliwa Donald Trump kuwa rais wa Marekani na pia Uamuzi wa Uingereza kutaka kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Jukwaa: Chama cha AfD kinataka kufunga mipaka ya Ulaya na kutaka kuwepo kwa ukaguzi wa vitambulisho katika mipaka ya ndani ya Ujerumani na pia wanataka kuzuia kuingia wageni na wakimbizi nchini Ujerumani. AfD piakinataka watu wote  waliokataliwa maombi ya ukimbizi  warudishwe makwao sambamba na kurudishwa makwao wakaazi wakigeni wanaoishi Ujerumani.

Mshirika anayependelewa ili kuunda serikali ya muungano: hakuna chama wanachotaka kuungano nacho lakini kinachokaribiana katika sera ni chama cha CDU

FREE DEMOCRATIC PARTY (FDP)

Kiongozi wa chama cha FDP Christian LindnerPicha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Rangi: Manjano

Kiongozi: Christian Lindner

Matokea ya uchaguzi wa 2013: Asilimia 4.8 viti: 0/630

Wanachama: 54,000

Wapiga kura: Wapiga kura wengi ni watu waliojiajiri wenyewe, hasa wafanya biashara, madaktari wa meno, wanasheria na wengineo.

Historia: Wana demokrasia huru walikuwa wakiwakilishwa katika bunge la Ujerumani tangu kuundwa kwa Shirikisho la Jamhuri 1949.

Chama hiki kiliundwa 1948 na kimeshiriki katika shirikisho la serikali kwa miaka 41, ni muda mrefu kuliko chama kingine chochote kile.

Jukwaa: Chama hicho lengo lake kubwa ni kuwepo kwa uhuru wa binafsi na haki za umma, japo kuwa kimefanya kampeni ya kutaka kuwepo kwa upunguzaji wa kodi, lakini hakitaki kujitoa katika soko la hisa.

Mshirika anayependelewa ili kuunda serikali ya muungano: CDU

 

 

Mwandishi: Knight, Benjamin/ Tafsiri: Najma Said

Mhariri: Saumu Yusuf

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW