1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatima ya dhabu ya kifo Marekani

Oumilkheir Hamidou
3 Aprili 2017

Kitandawili cha nani atagombea kiti cha kansela kwa tiketi ya chama cha Social Democratic (SPD) katika uchaguzi mkuu wa mwakani ndio mada iliyohodhi magazetini.

Mwenyekiti wa chama cha Social Democratic Sigmar GabrielPicha: Reuters/H. Hanschke

Tuanzie na suala linalojadiliwa kila pembe juu ya nani anafaa kukiongoza chama cha Social Democratic katika uchaguzi mkuu unaokuja. Gazeti la "Landeszeitung" la mjini Lüneburg linachambua shauri lililotolewa na mwenyekiti wa chama hicho, Sigmar Gabriel, na kusema: "Shauri la Gabriel ni zuri lakini pia ni hatari. Kiongozi wa SPD anataka ajitokeze mtu atakayeshindana naye chamani na kufika hadi ya kuzusha uwezekano wa wanachama kuulizwa maoni yao katika suala la nani anastahiki kuwa mgombea wa kiti cha kansela kwa tiketi ya chama cha SPD."

Mjadala wa nani akiongoze chama cha SPD katika uchaguzi mkuu 2017 wafunguliwa

Sigmar anahisi anaweza kugombea wadhifa wa kansela, anawajulisha wale wanaomkosoa. Lakini wamemnyamazia. Hakuna yeyote - si Steinmeier, si Scholz na wala si Schulz -anaetaka kukabiliana na zahma ya mwaka 2017.

Kwa vyovyote, kiongozi huyo wa SPD ameufungua mapema mjadala wa nani agombee kiti cha kansela. Kawaida chama husimama kidete nyuma ya mgombea wake. Lakini katika miaka iliyopita, SPD imekuwa mara kadhaa ikijitokeza kama chama kinachojichimbia wenyewe kaburi lake. Kwa hivyo, Gabriel anakabiliwa na mtihani wa miezi kadhaa akijua fika mwishowe atashindwa.

Magazetini yameangazia pia kuhusu Marekani na adhabu ya kifo. Gazeti la "Saarbrücker" linaandika kwamba ni jambo la kupongezwa kuwa Marekani hivi sasa haitoweza tena kutumia dawa yoyote ya sumu inayoruhusiwa na Idara ya Uchunguzi ya FDA kama chanjo kwa waliohukumiwa adhabu ya kifo "kwa sabahu makamampuni ya madawa ya Ulaya na Marekani yanapinga kuitengeneza."

Adhabu ya kifo yakabiliwa na changamoto

Madawa yanatakiwa yaokowe maisha ya binaadamu. Yeyote anayemtumilia mtu kinyume na matakwa yake anakwenda kinyume na mwongozo huo. Mwongozo ni dhahiri na bayana: Taifa, na hasa lile linalojibebesha jukumu la kuheshimu haki za binaadamu, linakuwa linatumia vibaya madaraka yake linaporuhusu sheria za adhabu ya kifo.

Ujerumani yaangushwa EuroVision

Hatimaye ni mashindano ya nyimbo barani Ulaya -EUROVISION - yaliyofanyika mjini Stockholm, Sweden, ambapo mwaka huu yameshuhudia ushindi wa mrembo kutoka Ukraine aliyeimba nyimbo dhidi ya kutimuliwa na kudhalilishwa watu wa jamii ya Tatar wakati wa enzi za Stalin nchini Urusi, huku Ujerumani imemaliza wa mwisho.

Gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linahisi ulikuwa uamuzi wa kisiasa. Gazeti linaendelea kuandika: "Bila ya shaka ni siasa. Iweje vyenginevyo pale nchi 42 kuanzia milima ya Ural hadi kufikia mwambao wa bahari ya Atlantik zinapokutana kwa mashindano? Mashindano ya Eurovision mwaka 2016 yaligubikwa na siasa kuliko mwaka wowote mwengine hapo awali."

Hata hivyo, siasa pekee haijawahi kuamua matokeo ya Eurovision. Anayetaka kushinda mashindanoni anabidi ang'are kiusanii. Ujerumani haikushindwa kwa sababu ya kuwa Ulaya imetaka kulipiza kisasi dhidi ya sera za Kansela Angela Merkel za kuacha milango wazi. Imeshindwa kwa sababu nyimbo nzuri iliyoimbwa na msichana mrembo aliyevalia nguo ya kupendeza, haikuwa ya kutosha

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/Inlandpresse

Mhariri: Mohammed Khelef

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW