1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nape akosolewa kwa matamshi yake makali

17 Julai 2024

Vyama vya siasa pamoja na wanaharakati nchini Tanzania vimekosoa na kulani vikali matamshi yaliyotolewa na waziri wa habari, Nape Mnauye kuhusu kutumia njia za udanganyifu ili kushinda uchaguzi.

Tanzania
Nape akosolewa kwa matamshi yake ya njia za kushinda uchaguziPicha: Zuberi Mussa

Waziri huyo amesema matokeo ya uchaguzi hayawezi kuamuliwa na kile kinachowekwa kwenye sanduku la kura pekee akisema kuna mbinu nyingine zinazoweza kumfanya mgombea kushinda.

Kiongozi wa chama cha wananchi CUF, Mohammed Ngulangwa mbali ya kuikosoa kauli hiyo lakini pia amesema ni kauli yenye kuudhi na kuleta ukakasisi katika taifa ambalo linajinadi kuimarisha demokrasia na kuzingatia utawala wa sheria.

Kauli hiyo imeibua hisia kali kutoka kwa makundi mbalimbali hasa wakati huu ambao taifa hilo likijiandaa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Waziri huyo alinukuliwa akisema matokeo ya uchaguzi hayawezi kuamuliwa na kile kinachowekwa kwenye sanduku la kura pekee akisema kuna mbinu nyingine zinazoweza kumfanya mgombea kushinda.

CCM yajiweka kando na matamshi ya Nape

Chama tawala nchini Tanzania CCM kikiongozwa na mwenyekiti wake na rais wa nchi Samia Suluhu HassanPicha: CCM office

Chama chake tawala CCM, kimetangaza kujiweka kando na kauli Nape na kwamba chama hicho hakiamini kushinda uchaguzi kwa mazingira ya utatanishi. Waziri Nape aliomba radhi kwa kauli hiyo.

Wachambuzi wa mambo wanaonya kuhusu kuendelea kuwaacha wanasiasa kutoa kauli zinazoweza kuwavunja moyo wapiga kura hasa kwa kuzingatia yale yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2019 wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 unaodaiwa kuchakachuliwa matokeo yake.

CCM yawaonya makada wake kuelekea mbio za uchaguzi

Chama chake tawala CCM, kimetangaza kujiweka kando na kauli hiyo ya mwanasiasa wake. Katibu wa uenezi na itikadi wa chama hicho, Amos Makalla amesema CCM haimani kushinda uchaguzi kwa mazingira ya kimezengwe zengwe.

Tayari mwenyewe Nape amejitokeza hadharani na kuomba radhi kuhusiana na kauli yake hiyo akisema aliifanya kwa masihara tu. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW