1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAQURA : Wanajeshi wa Ufaransa wawasili Lebanon

20 Agosti 2006

Wanajeshi 50 wa Ufaransa wamewasili kwa njia ya bahari kwenye mji wa kusini wa Naqura nchini Lebanon.

Hicho ni kikosi cha kwanza cha kimataifa kuwasili nchini Lebanon kuimarisha shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa katika eneo hilo.Ufaransa awali iliahidi kutuma wanajeshi 200 tu kuunda kikosi kilichoagizwa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa cha wanajeshi 15,000.Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mark Malloch amezitaka nchi za Ulaya kuongeza wanajeshi kuhakikisha kwamba kikosi hicho kinafikia lengo lake la kuwa na wanajeshi 3,500 kwenye eneo hilo katika kipindi kisichozidi siku 10.

Ujerumani imeazimia kusaidia kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa lakini haitotuma wanajeshi wa mapigano.

Ujerumani inaweza kupeleka manowari kusaidia kusimamia mpaka wa mwambao wa Lebanon na wanajeshi wa Bundeswehr wanaweza kutowa msaada wa shughuli ndogo ndogo kusaidia kikosi hicho.