1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Narendra Modi na Rais Tinubuwakutana mjini Abuja, Nigeria

17 Novemba 2024

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, leo anakutana na Rais wa Nigeria Bola Tinubu huku mataifa hayo makubwa ya Asia na Afrika yakishinikiza kuhusishwa zaidi katika masuala ya dunia

Mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ni kituo cha kwanza katika ziara ambayo itampeleka Waziri Mkuu wa India kwenye mkutano wa G20 nchini Brazil, na Guyana. Ziara hiyo inafanyika huku kukiwa na msukumo ulioanzishwa na India na Nigeria kuhusu uwakilishi wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Soma Pia: Benki ya Dunia yaiidhinishia Nigeria dola bilioni 1.57

Wanachama watano wa kudumu wa baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa ambao ni  Marekani, Urusi, China, Ufaransa na Uingereza kila mmoja ana kura ya turufu yenye nguvu. Katika miaka ya hivi karibuni, wafuasi wa sera ya kugawana mamlaka kwa usawa wamekuwa wakishinikiza kuongezwa nchi za Kiafrika, Asia na Amerika ya Kusini kwenye orodha ya wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW