1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaMarekani

NASA yarusha satelaiti za kuchunguza vimbunga vya kitropiki

Daniel Gakuba
8 Mei 2023

Taarifa za uchunguzi kutoka satelaiti hizo zitawawezesha wanasayansi kufahamu mahali vimbunga vitakapoelekea.

Futuristischer Weltraumsatellit in Erdumlaufbahn
Picha: Stanislav Rishnyak/Zoonar/NASA/picture alliance

Shirika la uchunguzi wa anga za juu la Marekani, NASA limepeleka angani satelaiti mbili ndogo, maalumu kwa kufuatilia vimbunga vya kitropiki kwa lengo la kuboresha utabiri wa hali ya hewa juu ya tufani.

Satelaiti hizo zimerushwa kutoka kituo kilichopo nchini New Zealand leo Jumatatu, na kitakuwa na uwezo wa kufanya tathmini ya kila saa, tofauti na zilizopo sasa zinazofanya hivyo kila baada ya masaa sita.

Mtaalamu kutoka shirika la NASA, Will McCathy ameuambia mkutano na waandishi wa habari kuwa taarifa za uchunguzi kutoka satelaiti hizo zitawawezesha wanasayansi kufahamu mahali vimbunga vitakapoelekea.

Aidha ukubwa wa vimbunga hivyo utabainika, hali itakayowasaidia wakaazi wa maeneo ya mwambao kujipanga vyema, na kuhamishwa kwa wakati ikibidi.