1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nasiriyah: Waziri wa Italia alinganisha shambulizi

13 Novemba 2003
Waziri wa ulinzi wa Italia leo, amezuru kituo cha mashambulizi ya bomu ya kujitolea muhanga maisha, ambayo yaliwaua Wataliani 18 nchini Iraq, akawalaumu wale wale walioendesha hujuma za tarehe 11 Septemba nchini Marekani. Waziri Antonio Martino aliwaambia waandishi habari, katika mji wa kusini mwa Iraq, Nasiriya kwamba Italia haitatishwa na shambulizi la jana. Mjini Roma hiyo jana, alisema anaamini wapiganaji wanaomtii kiongozi wa Iraq aliyepinduliwa Saddam Hussein wako nyuma ya shambulizi hilo. Hujuma za tarehe 11 Septemba zilifanywa na mtandao wa Waislamu wafuatao siasa kali al Qaeda.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW