1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO, EU zaapa uungaji mkono zaidi kwa Ukraine

Ruth Alonga10 Januari 2023

Jumuiya ya kujihami ya NATO na Umoja wa Ulaya zimeapa kuimarisha zaidi uungaji mkono wao kwa Ukraine kupambana na uvamizi wa Urusi na kuimarisha ushirikiano kati ya Ulaya na muungano unaoongozwa na Marekani.

Belgien, Brüssel | Unterzeichnung der 3. NATO-EU Kooperationsvereinbarung
Picha: Johanna Geron/REUTERS

Wakichochewa na vita vya Ukraine, maafisa wa ngazi ya juu wa NATO na Umoja wa Ulaya wameahidi kupanua ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili katika tamko la pamoja lililotiwa saini Jumanne mjini Brussels. Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg baada ya kutiwa saini makubaliano hayo katika makao makuu ya muungano huo wa kijeshi, pamoja na viongozi kadhaa wa Umoja wa Ulaya amesema   Ushirikiano kwa sasa ni muhimu zaidi kuliko hapo awali.

Soma pia:NATO na EU kushirikiana zaidi kufuatia uvamizi wa Ukraine

Na kwa upande mwingine rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya,Ursula Von der Leyen alikuwa na haya. "Vitisho na changamoto kutoka Urusi ni vitu vinavyoonekana hivi sasa, ingawa sio masuala pekee yaliyopo. Pia tulishuhudia China ikizidi kujaribu kuweka utaratibu mpya wa kimataifa kwa maslahi yake. Kwa hivyo lazima tuimarishe ustahimilivu wetu wenyewe. Na kwa tamko hili jipya la pamoja, pia tunaupeleka ushirikiano wetu katika  ngazi ngazi nyingine."

Muafaka wa ushirikiano umetiwa saini BrusselsPicha: Johanna Geron/REUTERS

Kwa mujibu wa Stoltenberg, Jumuiya hiyo ya Nato na Umoja wa Ulaya pia unalenga kuimaisha ushirikiano katika siku za baadae katika masuala yatakayotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi,anga za mbali, uingiliaji wa kigeni pamoja na kukabiliana na upotoshaji.Kadhalika Stoltenberg alizungumzia namna ambavyo China inazidi kutumia nguvu kuimarisha ushawishi wake na sera zake akisema ni changamoto inayopaswa kushughulikiwa. Stoltenberg alikumbusha  mkutano kati ya maafisa hao watatu saa chache baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka jana kuangazia uhusiano wao wa karibu.

Soma pia:NATO kujadili matumizi katika sekta ya ulinzi

Anadhani kuwa Rais Putin alitaka kuichukua Ukraine katika siku chache na kutugawanya. Kwa makosa yote mawili, ni wazi ameshindwa," alisema nakuongeza kuwa "Lazima tuendelee kuimarisha ushirikiano kati ya NATO na Umoja wa Ulaya na lazima tuimarishe zaidi msaada wetu kwa Ukraine,"

Azimio la Pamoja la Jumanne juu ya Ushirikiano wa NATO na umoja wa ulaya ni jaribio jipya la kuendesha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbele, ikiahidi kuboresha juhudi za ushirikiano ili kulinda miundombinu muhimu. Charles Michel ni Rais wa Baraza la Ulaya:

"Kuifanya Ulaya kuwa na nguvu kunaifanya NATO kuwa imara kwa sababu washirika wenye nguvu hufanya ushirikiano imara. Asante tena, mpendwa Jens, kwa kujitolea kwako katika kupeleka ushirikiano huu mbele. Unaweza kutegemea umoja wa ulaya. Asanteni."

Suala la kutanua ushirikiano rasmi baina ya  Taasisi hizo mbili,NATO na Umoja wa Ulaya ni changamoto kubwa hasa kwakuwa mwanachama wa NATO,Uturuki haiitambui Jamhuri ya Cyprus ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

afp, reuters, dpa

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW