NATO kuchunguza madai ya mauaji wa raia Libya
1 Aprili 2011Kulingana na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, dhamira ya operesheni ya kijeshi inayoendelea Libya ni kuwalinda raia wa kawaida. Itakumbukwa kuwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ilichukua hapo jana Alhamisi, usukani wa kuisimamia operesheni hiyo. Wakati huohuo, uongozi wa Uingereza unamhoji Waziri wa mambo ya nje wa Libya, Moussa Koussa, aliyekimbilia huko kutafuta hifadhi baada ya kuasi na kujiuzulu.
Mwanadiplomasia huyo amesisitiza kuwa Moussa Koussa anazungumza na maafisa wa serikali ya Uingereza kwa hiari na kwamba hajapewa kinga yoyote.Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Uingereza ,David Cameron, amesema kuwa kitendo hicho cha Moussa Koussa kuasi ni pigo kubwa kwa uongozi wa Kanali Muammar Gaddafi.
Wakati huohuo,Waziri wa Ulinzi wa Marekani , Bill Gates, ameirejelea tena kauli iliyotolewa na Rais Obama kuwa hakuna wanajeshi wowote wan chi kavu watakaoingia kwenye ardhi ya Libya.Hata hivyo waziri huyo aliepuka kuzielezea taarifa zilizotangazwa na vyombo vya habari kuwa maafisa wa shirika la ujasusi la Marekani la CIA wamekuwa nchini Libya kwa wiki kadhaa.