1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO kuimarisha uhusiano wake na washirika wa Asia

11 Julai 2024

Viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO leo wanalenga kuimarisha uhusiano na washirika wa Asia, baada ya kuikosoa China kwa kuwa mwezeshaji mkuu wa Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Washington, Marekani | Viongozi wa NATO wakiwa katika mkutano
Viongozi wa NATO wakiwa katika mkutanoPicha: Nathan Howard/REUTERS

Baada ya mkutano huo, viongozi hao pia watakutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, mwishoni mwa mkutano wa kilele wa NATO. 

Mkutano kati ya viongozi wa nchi 32 wa NATO, Umoja wa Ulaya na wale wa kanda ya Bahari ya Hindi na Pasifiki ambazo ni Australia, Japan, New Zealand na Korea Kusini unatarajiwa kuangazia kitisho kinachowekwa na China na Urusi kwa kanda zote mbili. 

Soma pia:Viongozi wa NATO wahitimisha mkutano wao wa kilele huko Marekani

Baadae macho yote yataelekezwa kwa Rais wa Marekani, Joe Biden, wakati akiufunga mkutano huo wa siku tatu uliogubikwa na mijadala ya masuala ya usalama na kusisitiza kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya uvamizi wa Urusi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW