Migogoro
NATO kujadili udhibiti wa nyuklia na utengezaji wa silaha
15 Juni 2023Matangazo
Brussels
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami-NATO Jenerali Jens Stoltenberg amesema mataifa ya muungano huo yatajadili namna ya kudhibiti nyuklia na mipango ya kuhifadhi silaha katika mikutano ijayo ya mawaziri wa ulinzi wa mataifa ya jumuiya hiyo.
Amesema kadhalika mawaziri hao wanapanga kujadili kupanua uwezo wa uzalishaji kwa silaha muhimu, jambo ambalo litatolewa uamuzi katika mkutano wa kilele wa NATO wa mwezi ujao.
NATO: Ukraine inapiga hatua katika uwanja wa mapambano
Mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO unatarajiwa kuanza leo hii Alhamisi kwa mazungumzo na wawakilishi kutoka sekta ya utengenezaji wa silaha na kamisheni ya NATO kwa Ukraine. Mada kuu ni vita inayoendelea ya Urusi dhidi ya Ukraine na matokeo yake.