1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO kutangaza jukwaa la ushirikiano na Ukraine

12 Julai 2023

Viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wanatarajiwa kutangaza jukwaa jipya la ushirikiano na Ukraine baada ya kushindwa kuipatia nchi hiyo tarehe ya uhakika ya kukaribishwa ndani ya muungano huo wa kijeshi.

NATO Gipfel in Litauen/Kommentarbild Selenskyj
Picha: Yves Herman/REUTERS

Tangazo hilo litatolewa baada ya mkutano kati ya viongozi wa nchi 31 wanachama wa NATO na Rais Volodomyr Zelenksy wa Ukraine, katika siku ya pili ya mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo unaofanyika kwenye mji mkuu wa Lithuania, Vilnius.

Soma pia: Zelensky akasirishwa na NATO kusuasua kuikubali Ukraine

Viongozi hao wanalenga kutangaza kuundwa kwa baraza la ushirikiano kati ya NATO na Ukraine, ambalo litakuwa chombo cha kudumu cha mashauriano baina ya pande hizo mbili lenye uwezo kuitisha mikutano nyakati za dharura.

Mpango huo ni sehemu ya juhudi za NATO za kuiweka karibu Ukraine ambayo viongozi wake wamefadhaishwa kwa kutopatiwa ratiba ya uhakika ya nchi hiyo kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo.

Badala yake NATO imesema Ukraine itajiunga na jumuiya hiyo pale wanachama watakapofikia mwafaka na mazingira yatakaporuhusu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW