1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO: Kuungwa mkono Ukraine ni jukumu muhimu

11 Julai 2023

Viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wanaokusanyika leo mjini Vilnius kwa ajili ya mkutano wao wa kilele wa siku mbili huku.

NATO Holds 2023 Summit In Vilnius
Picha: Celestino Arce/NurPhoto/picture alliance

Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na mvutano kuhusu Ukraine kujiunga na umoja huo baada ya Sweden kuujongelea zaidi katika jitihada yake kujiunga na umoja huo wa kijeshi. Katibu Mkuu wa NATO ameonesha kuwa na uhakika kwamba Uturuki itaufikisha ukingoni upinzani wake katika jitihada ya uanachama ya Sweden baada ya kukutana na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan na Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson.

Anasema jambo muhimu ni kwamba upo uhakika wa Uturuki kuridhia hatua hiyo. Hungary, ambayo bado haijaridhia itifaki ya kujiunga kwa Sweden, pia tayari imeonesha nia ya kusonga mbele.

Indo-Pasifik inahitaji ushirikiano zaidi na NATO.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol Picha: Chung Sung-Jun/AFP/Getty Images

Katika hatua nyingine Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amesema ushirikiano kati ya NATO na mataifa yalio katika ushirikiano wa  Indo-Pacifik kwa sasa ni  muhimu zaidi kuliko hapo awali. Akizungumza muda mfupi kabla ya kukutana na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg mjini Vilnius, Yoon alisema masuala ya usalama yanayoathiri maeneo hayo hayawezi kuwekwa kando na majadiliano haya ya sasa. 

"Kama Katibu Mkuu Jens Stoltenberg alivyosema, tuko katika hali ambayo usalama wa Atlantiki hauwezi kutenganishwa na usalama katika eneo la Indo-Pasifiki. Ushirikiano wa karibu kati ya NATO na mataifa ya Indo-Pacific kama vile Korea Kusini. Japan, Australia na New Zealand, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali."

Stoltenberg ndiye anaeongoza mkutano wa kilele wa wanachama wa NATO katika mji mkuu wa Lithuania katika siku mbili hizi yaani leo na kesho.

Hatma ya takwa la Ukraine kujiunga na NATO.

Ikumbukwe pia mwaka 2008 NATO iliridhia kuwa Ukraine inaweza kuwa mwanachama. Hata hivyo kanuni zenye kusimamia muongozo wa ushirikiano huo unazuia kulijumisha taifa ambalo lina mgogoro unaondelea. Kupitia ukurasa wake wa Twetter rais wa Ukraine, ambae anatarajiwa kushiriki mkutano huo Volodymyr Zelensky ameandika taifa lake lipo tayari kwa kujiunga na muungano huo.

Hata hivyo Stoltenberg amesema ana imana kuwa viongozi wa NATO watakubaliana katika namna chanya na kutoa ujumbe madhubuti kuhusu Ukraine kuelekea takwa la taifa hilo kujiunga na ushirikiano huo wa kijeshi. Katika mkutano huo pia mataifa washirika wanatarajiwa kuhitimisha mpango wa muda mrefu wa kuiunga mkono Ukraine katika kujikinga na mashambulizi. Na kadhalika kulifanya jeshi la taifa hilo kuwa la kisasa.

Soma zaidi:Uturuki yakubali kuiunga mkono Sweden kujiunga NATO

Baadhi ya mataifa yanatarajiwa kutoa ahadi za silaha na juhudi nyingine za usaidizi wa kiusalama kwa serikali ya Kiev. Kesho Jumatano ikiwa siku ya pili na ya mwisho ya mkutano huo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Marekani Joe Biden watafanya mkutano wa ana kwa ana na Zelensky ambao utajikita katika mipango ya kuiunga mkono Ukraine.

Chanzo: DPA

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW