NATO: Mashambulizi dhidi ya Wahouthi yalikuwa ya kujihami
12 Januari 2024Akizungumza leo, afisa huyo waNATO amesema pia mashambulizi hayo yalikusudiwa kudumisha uhuru wa shughuli katika Bahari ya Shamu, mojawapo ya njia muhimu zaidi za majini.
Amesema waasi wa Kihouthi wanafadhiliwa na kuungwa mkono na Iran, hivyo nchi hiyo ina wajibu maalum wa kuwadhibiti washirika wake.
Soma pia:Marekani na Uingereza zashambulia ngome za wahouthi, Yemen
Taarifa hiyo haijaeleza iwapo muungano huo wa kijeshi wenye nchi wanachama 31 unaunga mkono mashambulizi hayo. Wakati huo huo, nchi za Umoja wa Ulaya zitakutana wiki ijayo kujadili mpango wakuanzisha kikosi cha wanamaji kusaidia kulinda melikatika Bahari ya Shamu, kutokana na mashambulizi ya waasi wa Kithouthi wa Yemen.
Pendekezo hilo lilitolewa kabla ya Marekani na Uingereza hazijayashambuliwa maeneo ya Yemen yanayodhibitiwa na waasi wa Houthi.