1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yajadili hakikisho la usalama wa Ukraine baada ya vita

1 Juni 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wanaokutana mjini Oslo, Norway wanajadili njia za kuihakikishia Ukraine usalama wake baada ya kumalizika kwa vita baina ya Urusi na nchi hiyo.

Stoltenberg in Norwegen
Picha: Heiko Junge/IMAGO

Hata hivyo, zikisalia wiki takriban tano tu hadi kufanyika kwa mkutano wa kilele wa NATO, nchi wanachama wa jumuiya hiyo zina maoni yanayokinzana juu ya ombi la Ukraine kujiunga na NATO.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, akisaidiwa na nchi za Ulaya mashariki, anataka mkutano wa kilele wa Julai upeleke ujumbe mzito kwamba Ukraine itakuwa mwanachama wa NATO baada ya vita vya Urusi kumalizika.

Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg  amesema nchi zote wanachama zinakubaliana na ahadi ya mwaka 2018, kuwa siku moja Ukraine itakuwa mwanachama wa jumuiya hiyo ya kujihami.

Hata hivyo, wanadiplomasia wanasema Marekani yenye ushawishi mkubwa ndani ya NATO, haitaki kwenda mbali zaidi na ahadi hiyo yenye utata.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW