Washirika wa Magharibi wanaoiunga mkono Ukraine wanakutana Jumatano ikiwa ni siku ya pili kwa lengo la kuharakisha upelekwaji wa silaha nchini Ukraine ambayo pia inaomba ipatiwe ndege za kivita. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, amesisitiza kuhusu ombi lake la ndege za kivita kutoka kwa nchi za Magharibi, wakati ambapo Urusi ikianzisha mashambulizi katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine.