1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yajadili urasimishaji wa msaada kwa Ukraine

14 Juni 2024

Mawaziri wa ulinzi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wanakutana mjini Brussels kwa siku ya pili mfululizo kwa mazungumzo ya kurasimisha msaada wake kwa Ukraine.

Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami NATO Jens StoltenbergPicha: Dursun Aydemir/Anadolu/picture alliance / Anadolu

Nchi wanachama za Jumuiya ya NATO zimekuwa zikiratibu msaada kwa Ukraine kupitia
kundi lisilo rasmi, linaloongozwa na Marekani lakini sasa zinajadili njia za kubadilisha wajibu huo kwa miundo rasmi ya NATO.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amewaambia waandishi wa habari kwamba watajadili jinsi ya kuimarisha zaidi usalama unaozorota.

Zelensky ahimiza Ukraine isigawanywe na Urusi

"Tutajadili maendeleo yetu katika kuhakikisha kwamba mipango yetu ya ulinzi ni thabiti na iko tayari kutekelezwa. Tutashughulikia uzalishaji wa viwanda vya ulinzi ili kuhakikisha utekelezaji muhimu unaohitajika kwa ulinzi wetu na kuendelea kuiunga mkono Ukraine."

Aidha mawaziri hao wanatarajiwa kuunga mkono mpango wa Ujumbe unaoitwa Msaada wa Usalama wa NATO na Mafunzo kwa Ukraine (NSTU) ambayo tayari kufikia siku ya Alhamisi ulikuwa umeidhinishwa katika kiwango cha chini.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW