NATO yajiandaa kwa hatari ya vita na Urusi
9 Februari 2024Maafisa wa juu wa kijeshi katika jumuiya hiyo ya NATO walionya hivi kaibuni kwamba Muungano huo unahitaji kujitayarisha kwa mgogoro mkubwa na Urusi.
Kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ulioanza miaka miwili iliyopita, gazeti la kila siku la mjini Oslo, Dagbladet, liliripoti kwamba Mkuu wa Jeshi la nchi hiyo, Jenerali Eirik Kristoffersen, amesema kwa sasa kuna muda wa kama miaka miwili au mitatu ambao lazima jumuiya hiyo iwekeze zaidi katika kuimarisha jeshi lake la ulinzi.
Soma zaidi: Ukraine, Urusi zaidi kudunguliana ndege zisizotumia rubani
Huku hayo yakiarifiwa, kamanda wa jeshi wa taifa jirani la Sweden, Micael Byden, alitoa wito kwa washirika wake na wanasiasa kuondoka kutoka kuelewa na wasogee zaidi katika kuchukua hatua.
Soma zaidi: Zelenskiy asema vikosi vyake vyazidi kushangaza
Hata hivyo, wataalamu wanaliona hili kama ombi kutoka kwa viongozi wa kijeshi kwa wanasiasa wa Ulaya ili kupata mabadiliko ya kimkakati katika mgogoro wa Urusi.
Katika mahojiano na DW, mtaalamu wa masuala ya usalama wa Ujerumani, Nico Lange, amesema matumaini ya kumalizika vita vya Ukraine bila mavurugano makubwa hayajafikiwa.
Ukraine imekuwa ikipokea msaada wa kijeshi kutoka kwa washirika wake wa Magharibi huku Urusi ikiwekewa vikwazo.
Uhaba wa silaha
Zaidi ya yote, viongozi hao wa kijeshi na wachambuzi wa mambo wana wasiwasi kuhusu uhaba wa silaha za kisasa na pia kuongezeka kwa utengenezaji wa silaha hasa barani Ulaya.
Mwaka uliopita, Umoja wa Ulaya uliahidi kutoa silaha zaidi kwa Ukraine ifikapo mwezi Machi, lakini ahadi hiyo haikufanikishwa.
Soma zaidi: Zelensky ahimiza nchi wanachama wa EU na Marekani kuipa Ukraine misaada zaidi ya kifedha
Kulingana na Lange, anayejishughulisha pia na masuala ya Mkutano wa Usalama wa Munich, sababu moja ni kwamba Ujerumani ilichukua muda mrefu kutoa dhamana kwa wazalishaji.
Lange alisema NATO ina miaka mitano pekee ya kuimarisha nguvu zake kijeshi kwa kuwa na silaha za kutosha ili kuhakikisha inaweza kuzuwiya mashambulizi ya Urusi dhidi ya mataifa wanachama wa NATO.
Katika hivi vita vya Ukraine kwenye kipindi hiki cha pili cha baridi, viongozi wa kijeshi na wachambuzi wanajikita katika uhaba wa silaha ilionao Ukraine katika vita vyake na Urusi.
Inaonekana Urusi inaweza kuziba pengo lake la silaha kutoka kwa Korea Kaskazini, huku Ukraine ikilazimika kupata silaha hizo kwa mgao.
Mabadiliko kwenye mkakati
Mchambuzi mwengine wa masuala ya kisiasa, Michael Kofman, alisema inawezekana kwamba wanajeshi wa Ukraine inabidi waondoke katika mji wa mashariki wa Avdiika na pia kuna hatari ya Urusi kushambulia zaidi katika mji wa Kupiansk ulio upande wa kaskazini.
Katika mahojiano ya radio, Christian Mölling, Mkuu wa Shirika la Usalama na Ulinzi katika Baraza la Masuala ya Kigeni la Ujerumani alisema kwa sasa iko wazi kabisa kwamba Ukraine kucheleweshwa kupata silha na vifaa vyengine vya kijeshi ndani ya miaka miwili iliyopita, kunamaanisha inabidi wanajeshi wake waondoke katika maeneo waliyoyakomboa.
Soma zaidi: Mwanadiplomasia mkuu wa Latvia ataka nafasi ya juu NATO, akiahidi maono ya wazi kuhusu Urusi
Hata hivyo, katika kuelekea mkutano wa kilele wa wataalamu wa kijeshi wa nchi za Magharibi unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo katika Mkutano wa Usalama wa Munich, Lange anaamini kwamba huenda "tukaona mwanzo wa mabadiliko ya mkakati na hili limechochewa na hali ya kijeshi nchini Ukraine."