NATO yaonya juu ya uhaba wa risasi Ukraine
14 Februari 2023Amesema NATO itaongeza malengo yake ya ugavi wa silaha, huku kukiwa na upunguaji wa haraka wa hesabu yake katika vita vya Ukraine, na ametoa wito wa uwekezaji katika uwezo wa uzalishaji.
Stoltenberg pia amesisitiza kwa mara nyingine tena uungaji mkono wa NATO kwa Ukraine.
Soma pia:NATO yairai Korea Kusini juu ya msaada Ukraine
Ugavi wa risasi umekuwa jambo la kutia wasiwasi kwa vikosi vya Ukraine na Urusi kwa miezi kadhaa.
Wakati huo huo Stoltenberg amegusia pia masuala mengine kuhusu vita hivyo, na kusema miongoni mwa mambo mengine, kwamba anatarajia utoaji wa ndege za kivita za NATO kwa Ukraine, kuwa mada ya majadiliano kwenye mkutano unaofanyika leo Jumanne.
Serikali ya Ukraine imekuwa ikitoa wito wa kupatiwa ndege za kivita za magharibi tangu kuanza kwa mzozo huo.