1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO ina imani na juhudi za Marekani kusitisha vita Ukraine

2 Desemba 2025

Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte amesema ana imani kuwa juhudi za Marekani za kuvimaliza vita vya Ukraine zinaweza kuleta amani.

Belgien Brüssel 2025 | NATO-Generalsekretär Mark Rutte bei Pressekonferenz
Picha: Yves Herman/REUTERS

Rutte ameyasema haya wakati ambapo mjumbe maalum wa rais wa Marekani Steve Witkoff yuko mjini Moscow kukutana na Rais Vladimir Putin.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Rutte amesema NATO inakaribisha juhudi zinazoendelea za kuleta amani zikiongozwa na Marekani.

Rutte ameyatoa matamshi haya huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akisema kuwa wajumbe wa Marekani na Ukraine wameubadili mfumo wa mkataba wa amani uliobuniwa mjini Geneva, wakati wa mazungumzo yao ya hivi karibuni yaliyofanyika Florida, Marekani.

Zelenskiy vile vile amesema kuwa anataka mataifa rafiki wa Ukraine barani Ulaya wajumuishwe zaidi katika mchakato huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW