1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yashindwa kuidhinisha mpango mpya wa ulinzi

16 Juni 2023

Mawaziri wa ulinzi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO leo wameshindwa kupata mwafaka kuhusiana na mipango mipya ambayo jumuiya hiyo itatumia kujibu shambulizi la Urusi.

Viongozi wa NATO
Viongozi wa NATOPicha: Yves Herman/REUTERS

Mwanadiplomasia mmoja ameilaumu Uturuki kwa kukosekana kwa maelewano hayo. Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema mawaziri hao waliangazia upya mipango hiyo, hiyo ikiwa mara ya kwanza tangu mwisho wa Vita Baridi, hatua iliyochochewa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Stoltenberg awali alisema kwamba mawaziri hao wanakaribia kuelewana. Hatua hiyo inaashiria mabadiliko makubwa ya kimsimamo kwa NATO kwa kuwa jumuiya hiyo awali ilikuwa haioni haja ya kuwa na mipango mikubwa ya kujilinda, kwa kuwa ilikuwa inapigana vita vidogo nchini Afghanistan na Irak na ilihisi kwamba Urusi haina kitisho chochote baada ya utawala ule wa Umoja wa Sovieti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW