1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yathibitisha kisa cha mtandao kulenga tovuti zao

13 Februari 2023

Jumuiya ya Kujihami ya NATO imethibitisha tukio la mtandao lililoathiri tovuti zao usiku wa kuamkia leo.

Belgien NATO l Treffens der Verteidigungsminister l Stoltenberg
Picha: Kenzo Tribouillard/AFP

Afisa mmoja wa NATO ameliambia shirika la habari la Ujerumani DPA, kwamba wataalamu wa jumuiya hiyo wa masuala ya mitandao wanalishughulikia tukio hilo linaloathiri baadhi ya tovuti.

Kauli hiyo imejiri baada ya ripoti za mitandao ya kijamii kudokeza kwamba huenda wadukuzi wenye mafungamano na Urusi wamedukua tovuti ya makao makuu ya operesheni spesheli za  NATO  (NSHQ).

Kundi la udukuzi la Urusi Killnet, lilidaiwa kuhusika na shambulizi hilo la mitandao. Kundi hilo limewahi kuhusishwa na visa vingine vya udukuzi, ikiwemo Ujerumani kwa kulenga tovuti za bunge, polisi na miundombinu muhimu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW