1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Navalny atumia ujanja kupata taarifa za jaribio la kumuua

Zainab Aziz Mhariri: Mohammed Khelef
22 Desemba 2020

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi, Alexei Navalny, ameeleza jinsi alifanikiwa kumtia mtegoni jasusi wa Urusi aliyekiri kwamba maafisa wa usalama walitaka kumuua kwa kutumia na sumu.

Russland I Nawalny
Picha: Shamil Zhumatov/REUTERS

Patashika hiyo inaonekana kama sinema ya James Bond. Huwezi kuamini kama matukio hayo ni halisi katika maisha ya kiongozi wa upinzani wa Urusi, Alexei Navalny, ambaye kwa sasa anaendelea kupata ahueni nchini Ujerumani.

Inaaminika kwamba baada ya kupewa sumu, hatimaye ameweza kuwasiliana na kurekodi mahojiano na mmoja wa majasusi kutoka Idara ya Usalama wa Taifa nchini Urusi (FSB) ambaye anafahamu fika juu ya jaribio la kuyatoa maisha ya kiongozi huyo wa upinzani.

Soma Zaidi:Kisa cha Navalny kulishwa sumu chazidisha wasiwasi

Kama ilivyodhihirishwa na jukwaa la uchunguzi la waandishi wa habari, Bellingcat, katika mazungumzo marefu kati ya Navalny na ofisa wa ujasusi, ambaye kwa mujibu wa kiongozi wa upinzani alijitambulisha kwa jina la Konstatin Kudryavtsev, ofisa huyo alikiri kwamba FSB kweli ilihusika na kitendo cha kumwekea sumu Navalny, jambo ambalo maafisa wa Urusi hadi sasa wanaendelea kulikana.Kwenye mahojiano hayo ya kusisimua, Navalny aliuliza iwapo mpango mzima ulikuwa mauti yamkute katika hoteli au kwenye ndege? Afisa  wa ujasusi Kudryavstsey alijibu, hakuwa na taarifa yoyote juu ya hilo.

Rais wa Urusi Vladmir PutinPicha: Alexei Druzhinin/dpa/picture-alliance

Baadae Navalny alichapisha video iliyomuonyesha akizungumza kwa simu kwenye akaunti yake ya YouTube na kuipa jina "Nilimpigia simu muuaji wangu - Amekiri."

Kiongozi huyo wa upinzani ambaye pia ni mwanaharakati anayeipinga serikali ya Urusi alisema huo ni ushahidi wa kutosha kwamba serikali ilitaka kumuua lakini amesema hatafungua mashtaka bali atauwasilisha ushahidi huo kwa raia wa Urusi.

Chanzo: https://p.dw.com/p/3n1eg

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW