Nawaz Sharif aapa kuuangamiza utawala wa kiimla Pakistan
26 Novemba 2007Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif, ameapa atasaidia kuuangamiza utawala wa kiimla nchini Pakistan.
Kiongozi huyo amesema atawasilisha hati yake ya uteuzi ili aweze kugombea katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 8 mwezi Januari mwakani.
Hata hivyo Nawaz Sharif, aliyerejea jana nchini Pakistan kutoka uhamishoni nchini Saudi Arabia, ametishia kuugomea uchaguzi huo iwapo rais Pervez Musharraf hataondoa utawala wa hali ya hatari.
Amesema amerejea nchini Pakistan kuwahudumia wanananchi na kuliokoa taifa. Wafuasi wake wanaamini yeye ndiye kiongozi pekee anayeweza kuikoa Pakistan.
Kurejea kwa Nawaz Sharif, aliyetimuliwa na rais Musharraf miaka minane iliyopita, kunaongeza shinikizo dhidi ya jenerali Musharraf amalize utawala wa hali ya hatari nchini Pakistan.