1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi 40 zaitaka China kuheshimu haki za binaadamu

Sylvia Mwehozi
7 Oktoba 2020

Takriban nchi 40 zimeitaka China kuheshimu haki za binaadamu za watu wa jamii ya Uighur. Wito huo wa pamoja umetolewa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binaadamu.

Türkei Protest gegen Uiguren-Politik in China
Picha: Getty Images/AFP/O. Kose

Balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa, Christoph Heusgen amesema wanaitaka China kuheshimu haki za binaadamu hasa za makabila ya watu wachache pamoja na dini, kwenye majimbo ya Xinjiang na Tibet. Miongoni mwa nchi 38 zilizosaini wito huo ni pamoja na Marekani na nchi nyingi za Umoja wa Ulaya ikiwemo Albania na Bosnia, pamoja na Canada, Haiti, Hondurus, Japan, Australia na New Zealand. Nchi hizo pia zimeelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya Hong Kong. Hata hivyo, balozi wa Pakistan alisimama na kusoma taarifa iliyosainiwa na nchi 55 ikiwemo China, inayolaani unafiki wa nchi zinazoitumia hali ya Hong Kong kama kisingizio cha kuingilia masuala ya ndani ya China.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW