1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Nchi kadhaa zasitisha ufadhili kwa UNRWA

29 Januari 2024

Ujerumani na nchi nyingine nane tayari zimetangaza kuwa kwa sasa, zinasitisha ufadhili wao kwa shirika la UNRWA linalotoa misaada Gaza.

Madai kwamba wafanyakazi wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza UNRWA walihusika katika shambulizi la Oktoba 7 dhidi ya Israel, yazidi kuzusha ghadhabu.
Madai kwamba wafanyakazi wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza UNRWA walihusika katika shambulizi la Oktoba 7 dhidi ya Israel, yazidi kuzusha ghadhabu.Picha: picture alliance/dpa/APA/ZUMA Press Wire

Baada ya baadhi ya nchi kuamua kukata ufadhili, wawakilishi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu waliitisha mkutano wa dharura mjini Cairo Jumapili kuhusu vita hivyo na mgogoro wa kibinadamu unaoendelea Gaza.

Mwakilishi wa kudumu wa Mamlaka ya Wapalestina katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Muhannad al-Aklouk, alilaani kukatwa kwa ufadhili wa UNRWA na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuendelea kufadhili shirika hilo.

"Tunakataa uamuzi wowote kutoka kwa nchi yoyote kuhusu kukata au kupunguza ufadhili wao kwa UNRWA. Nchi zote zinapaswa kuwa za haki na kuangalia mambo kwa kiwango kimoja na si kwa kuegemea upande fulani," amesema Muhannad al-Aklouk.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia ameyatolea wito mataifaambayo yamesitisha michango yao akisema ipo haja ya kuhakikisha kazi ya UNRWA inaendelea.

Israel yazidi kushinikizwa kusitisha mapigano Gaza

Guterres amesema tisa kati ya washukiwa 12 tayari wameshatambuliwa na kwamba wamesimamishwa kazi mara moja.Picha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Guterres: Hatua za kisheria kuchukuliwa

Madai kuwa wafanyakazi 12 wa UNRWA walihusika kwenye shambulizi la kigaidi lilifofanywa na wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, yametia shinikizo kubwa dhidi ya shirika hilo.

Guterres ameahidi kuchukua hatua za kisheria kufuatia madai kwamba wafanyakazi wa shirika lake la misaada katika Ukanda wa Gaza UNRWA walihusika na mashambulizi ya kigaidi ya Oktoba 7 yaliyofanywa na wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel.

Kulingana na taarifa kutoka Umoja wa Mataifa iliyotolewa na Antonio Guterres siku ya Jumapili, mfanyakazi yeyote wa Umoja wa Mataifa anayehusika na matendo ya kigaidi atawajibishwa, ikiwemo kufunguliwa mashtaka ya jinai.

Matukio yanayoendelea katika vita vya Israel-Hamas

Tayari ofisi inayohusika na Huduma za Uangalizi wa Ndani katika Umoja wa Mataifa imeanzisha uchunguzi dhidi ya madai hayo.

Vikosi vya Israel vilivyoko Gaza vimeripoti kutokea mapigano makali eneo la Khan Younis Picha: Ohad Zwigenberg/AP/picture alliance

Israel, Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine kadhaa huliorodhesha Hamas kuwa kundi la kigaidi.

Vikosi vya Israel kusitisha mapigano kwa saa nne kuanzia Jumapili hadi Jumanne

Kwingineko, vikosi vya Israel vilivyoko Gaza vimeripoti kutokea mapigano makali eneo la Khan Younis kusini mwa ukanda wa Gaza, ambako vikosi hivyo vilipata silaha nyingi. Hayo ni kulingana na taarifa waliyochapisha kwenye ukurasa wao wa mtandao wa X.

Israel yazidisha mashambulizi baada ya askari wake kuuawa

Msemaji wa jeshi la Israel alitoa wito mpya kwa Kiarabu kuwataka watu wanaoishi katika baadhi ya maeneo ya Khan Younis kuondoka eneo maalum katika pwani ya Mediterania.

Hospitali katika Ukanda wa Gaza zaelemewa

02:03

This browser does not support the video element.

Alitangaza usitishaji vita wa kimkakati kwa muda wa saa nne kila siku kuanzia Jumapili hadi Jumanne ili kuwezesha watu katika eneo la Rafah kuondolewa na kudhibitiwa kwa maeneo yanayolengwa.

Takriban watu 1,200 waliuawa kwenye shambulizi la Hamas kusini mwa Israel na zaidi ya 240 walichukuliwa mateka na kupelekwa Gaza, baadhi hawajaachiliwa hadi wa leo.

Chanzo: DPAE