1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi masikini zakasirishwa na matajiri mkutano wa Doha

6 Machi 2023

Viongozi kutoka nchi masikini kabisa duniani wameonesha hasira na kuvunjwa moyo katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa, kuhusiana na namna nchi zao zinavyoangaliwa na mataifa tajiri.

Katar, Doha | UN LDC5 Konferenz
Picha: Mohammed Dabbous/AA/picture alliance

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadéra ameuambia mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa nchi masikini kabisa duniani, unaofanyika Doha kwamba nchi yake ina rasilimali, lakini ni masikini kutokana na mali zao kuporwa na nchi zenye nguvu za Magharibi. 

''Jamhuri ya Afrika ya Kati siku zote imekuwa ikiangaliwa na baadhi ya nchi za Magharibi zenye nguvu kama hifadhi ya rasilimali ghafi za kimkakati. Tangu ilipopata uhuru wake imekuwa ikilengwa na uporaji unaosaidiwa na ukosefu wa hali ya uthabiti'' alisema Touadera.

Aidha, mabenki ya kimataifa yamekosolewa kwenye mkutano huo kwa kuziwekea nchi masikini viwango vikubwa vya riba katika mikopo wanayochukuwa.

Miito pia imetolewa kwenye mkutano huo wa kuyataka mataifa makubwa yaliyoendelea kutowa mabilioni ya dola waliyoahidi kama msaada wa kuzisaidia nchi zisizojiweza kuepuka umasikini na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW