1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi nyingi maskini bado hazijapokea chanjo ya corona

13 Mei 2021

Wakati mataifa tajiri yakihifadhi chanjo za covid-19 kwa ajili ya raia wao, nchi nyingi masikini bado zinahangaika ili kupata dozi za chanjo hizo, miongoni mwake zimo za kiafrika.

Ghana | AstraZeneca | COVAX-Impfstoff
Picha: Francis Kororoko/REUTERS

Katika hospitali ndogo iliyopo katika mji mkuu wa Chad hakuna mjadala wa ni chanjo gani ni bora zaidi kuliko nyengine sababu kuu; Hakuna chanjo kabisa.

Hakuna chanjo hata ya madaktari au wauguzi wanaoshughulikia wagonjwa walioambukizwa Covid 19 nchini Chad, nchi ambayo thuluthi moja ya eneo lake imefunikwa na jangwa la Sahara.

Dkt. Oumaima Djarma daktari wa magojwa yanayoambukizwa nchini humo amesema anashangazwa na hali hiyo na anaiona sio haki lakini anaongeza kuwa hawana la kufanya na chanjo yoyote iliyoidhinishwa itakayowafikia wataitumia.

Wakati mataifa tajiri yakiendelea kuhifadhi chanjo, mataifa mengi maskini bado yanagombania kupata chanjo na miongoni mwao kama taifa la Chad, Bukina Faso, Burundi, Eritrea na Tanzania hayajapata kabisa.

Madagscar nayo imepokea chanjo kupitia COVAXPicha: Alexander Joe/AP Photo/picture alliance

Shirika la Afya Ulimwenguni limeonya kuwa uhaba na kucheleweshwa kwa usambazaji wa chanjo unapelekea matiafa ya Africa kurudi nyuma zaidi katika usambazaji na utoaji wa chanjo na kuliweka bara hilo kuwa na asilimia 1 ya waliochanjwa.

Gian Gandhi, Mratibu wa idara ya Ugavi wa mpango chanjo - COVAX wa shirika la UNICEF amesema kuna uwezekano wa kuibuka kwa aina mpya ya virusi katika maeneo ambayo hayajapokea chanjo na kutoa wito kwa matiafa tajiri kusaidia mataifa ambayo hayajapokea dozi kufikia sasa.

Chad imethibitisha vifo 170 pekee tangu janga hili lianze, lakini juhudi za kukomesha virusi kabisa hazijafanikiwa. Ingawa uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji mkuu wa nchi hiyo, Ndjamena ulifungwa kwa muda mfupi mwaka jana, kisa cha kwanza cha maambukizi  kilikuja kupitia mtu ambaye alivuka mmoja ya mipaka ya Chad kinyume cha sheria.

Mpango wa COVAX unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa  wa kusambaza chanjo duniani unalenga kusaidia mataifa yenye kipato cha wastani na cha chini kupata huduma hiyo.

Ethiopia ni miongoni mwa nchi zilizopokea chanjo kupitia COVAXPicha: Amanuel Sileshi/AFP

Chad inatarajiwa kupokea chanjo ya Pfizer mwezi ujaoiwapo itaweza kutenga vyumba vya baridi ambavyo vinahitajika katika kuhifadhi chanjo hio kwa usalama. Baadhi ya mataifa yameshindwa kufikia mahitaji ya kupokea dozi kutokana na sababu mbalimbali za watengezezaji wa chanjo.

Nchina Burkina Faso nako wahudumu wa Afya waliokatika mstari wa mbele wanasema hawana uhakika kwanini serikali haijapokea chanjo kufikia sasa.

Nchini Haiti hakuna hata chanjo moja iliyopelekwa licha ya kuwa na watu zaidi ya milioni 1. Haiti iliratibiwa kupokea dozi 756 elfu ya chanjo ya AstraZeneca kupitia mpango wa COVAX lakini maafisa wa serikali wanasema hawakuwa na muundo mbinu wa kuihifadhi.

Visiwa kadhaa vidogo katika bahari ya Pasifiki pia havijapokea chanjo yoyote, ingawa kutokuwepo milipuko wa janga la corona katika visiwa vingine inamaanisha hakuna uharaka wa kampeni za chanjo

Vanuatu, kisiwa chenye idadi ya watu 300,000, inasubiri kupokea dozi ya kwanza ya chanjo ya AstraZeneca baadaye mwezi huu, ilirekodi visa vitatu tu vya virusi vya Corona, na wote wakawekwa karantini.