Nchi za EU zatakiwa kuionyesha Ukraine kuwa zinaiunga mkono
19 Machi 2026
Matangazo
Mkuu huyo wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, amesema Jumuiya hiyo inapaswa kuionyesha Ukraine uungaji wake mkono wakati ambapo Rais wa Hungary Viktor Orban anapoendelea kuzuia mkopo unaohitajika sana na serikali ya Kiyv kutokana na nchi hizo mbili kuwa kwenye mvutano.
Kallas aliwaambia waandishi wa habari alipowasili katika eneo la mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels ambako viongozi hao wanatarajia kuidhinsiha ufadhili wa euro bilioni 90 ambazo Hungary ilisaini mwezi Desemba pamoja na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Ulaya.