1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za G7 zalaani ushirikiano wa Korea Kazkazini na Urusi

6 Novemba 2024

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la nchi saba tajiri duniani la G7 pamoja na nchi nyingine, wamelaani kuongezeka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini na Urusi.

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G7 katika picha ya pamoja iliyochukuliwa mnamp Aprili 18,2024 mjini Capri kusini mwa Italia walipokutana kwa kongamano la siku tatu kujadili msaada kwa Ukraine
Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G7Picha: Alessandro di Meo/EPA

Katika taarifa ya pamoja, wanadiplomasia hao walielezea wasiwasi wao kuhusu kupelekwa kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi, huku kukiwa na uwezekano wa kutumika kwa wanajeshi hao katika uwanja wa vita nchini Ukraine.

Viongozi wa G7 wakamilisha mkopo wa Ukraine uliotokana na mali za Urusi

Taarifa hiyo imeongeza kuwa uungaji mkono wa moja kwa moja wa Pyongyang katika vita vya uchokozi vya Urusi dhidi ya Ukraine, mbali na kuonyesha juhudi za kukata tamaa za Urusi kufidia hasara zake, utaashiria kutanuka kwa mzozo huo na kusababisha athari kubwa kwa amani na usalama wa Ulaya na eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki.

Taarifa hiyo ilitiwa saini na nchi za G7 pamoja na Australia, Korea Kusini, New Zealand na mjumbe mkuu wa Umoja wa Ulaya.