1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za G7 zamuunga mkono kiongozi wa upinzani wa Venezuela

Josephat Charo
27 Novemba 2024

Venezuela imesema itadurusu upya mahusiano yake na nchi za G7. Nchi wanachama zikiwemo, Italia na Marekani tayari zimemtangaza Gonzalez Urrutia tkuwa rais mteule wa Venezuela.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za G7 katika mkutano wao nchini italia
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za G7 katika mkutano wao nchini italiaPicha: Claudia Greco/REUTERS

Nchi zilizostawi kiviwanda na zinazoinukia kwa kasi kiuchumi duniani za G7 zimechochea jawabu la ghadhabu kutoka kwa serikali ya mjini Caracas jana Jumanne kwa kuyaunga mkono madai ya kiongozi wa upinzani wa Venezuela Edmundo Gonzalez Urrutia kwamba alishinda uchaguzi uliofanyika mwezi Julai mwaka huu.

Kundi hilo linalozijumuisha Marekani, Canada, Italia, Ujerumani, Uingereza, Japan na Ufaransa, zimesema kwenye taarifa kwamba umma wa Venezuela ulifanya chaguo la wazi na kumpigia kura Gonzalez kwa wingi mkubwa wa kura kwa mujibu wa rekodi za uchaguzi zilizopo.

Baada ya mkutano wao wa siku mbili katika mji wa Fiuggi nchini Italia nchi za G7 ziliunga mkono kipindi cha amani cha mpito Venezuela na kuelezea wasiwasi wao kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW