1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za G7 zasisitiza kuendelea kuiunga mkono Ukraine

17 Novemba 2024

Viongozi wa kundi la nchi saba zilizoendelea kiviwanda, G7, wamesisitiza ahadi yao ya kuendelea kuiwajibisha Urusi vikali kwa uvamizi wake nchini Ukraine

Italien | G7 Gipfel in Borgo Egnazia | Giorgia Meloni
Picha: Andrew Medichini/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, ambaye ni mwenyekiti wa kundi la G7 mwaka huu, ameihakikishia Ukraine kuhusu uungwaji mkono usioyumbayumba wa mataifa hayo.

Viongozi wa Marekani, Canada, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Italia na Japan wamesema Urusi bado ni kizuizi pekee cha amani ya kudumu. Wamesema Urusi itaendelea kukabiliwa na vikwazo na udhibiti wa mauzo ya nje kutoka kwenye nchi za Magharibi na washirika wake.

Soma Pia: Viongozi wa G7 kujadili uhamiaji, Afrika na akili mnemba

Wakati huo huo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema nchi yake ingependa kuvimaliza vita mwaka ujao kwa njia za kidiplomasia. Maoni yake ni kutokana na kutokuwa na uhakika juu ya mwelekeo wa baadaye wa vita hivyo.

Rais wa mteule wa Marekani, Donald Trump, ameapa kusitisha mapigano atakapoingia madarakani mwezi Januari. Siku ya Jumanne, Ukraine itaadhimisha siku 1000 tangu Urusi ilipoivamia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW