1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za Ghuba zaomboleza kifo cha rais wa Iran

20 Mei 2024

Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Waziri wake wa Mambo ya Nchi za Nje Hossein Amir-Abdollahian na maafisa wengine, wamepatikana wamekufa katika eneo la ajali ya Helikopta iliotokea hapo jana.

Saudi Arabia | mkutano wa kilele mjini Riyadh
Raisi akiwa katika mmoja ya mikutano ya kikanda nchini Saudi ArabiaPicha: WANA NEWS AGENCY/REUTERS

Majirani wa Iran katika nchi za Guba wameendelea kuomboleza kifo cha rais wa Jamhuri hiyo ya kiislamu Ebrahim Raisi pamoja na Waziri wake wa mambo ya nje Hossein Amir-Abdollahian katika ajali ya helikopata Magharibi mwa Iran.

Saudi Arabia, iliyoyarekebisha mahusiano yake na taifa hilo mwezi uliopita baada ya mvutano wa muda mrefu, ilitoa salamu zake za rambirambi kwa kiongozi wa juu wa taifa Iran  Ayatollah Ali Khamenei na kaimu rais Mohammad Mokhber kwa kifo cha rais wao pamoja na maafisa wengine wa serikali walioangamia katika ajali hiyo.

Soma pia: Tanzia Ibrahim Raisi: Rais mwenye msimamo mkali mwenye ukaribu na Ayatollah Khamenei

 Rais wa Umoja wa Fame za kiarabu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan imesema nchi yake iko pamoja na Iran katika wakati huu mgumu. Nye mtawala wa Qatar Tamim bin Hamad Al-Thani amesikitishwa na kifo cha rais huyo alichokiita cha uchungu na kutoa mkono wa pole kwa serikali na watu wa Iran kwa Ujumla.

Mfalme wa Bahrain  Hamad bin Isa Al Khalifa, Katibu Mkuu wa Baraza la ushirikiano la nchi za Guba GCC Jassem al-Budaiwi, Sultan wa Oman Haitham bin Tariq al-Said na kiongozi wa  Kuwait Sheikh Meshal al-Ahmad Al-Sabah wote walitoa salamu zao za rambirambi kwa Iran kwa kifo cha rais Ebrahim Raisi pamoja na maafisa wake 8 wa serikali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW