1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za kiarabu na kiislamu zataka ´kuisusa´ Israel

16 Septemba 2025

Viongozi wa mataifa ya kiarabu na kiislamu wametoa mwito wa kupitiwa upya mahusiano yao na Israel kufuatia shambulizi kubwa lililofanywa na nchi hiyo dhidi ya viongozi wa Hamas kwenye mji mkuu wa Qatar wiki iliyopita.

Viongozi wa kiarabu na kiislamu wakiwasili Doha, Qatar kwa mkutano wa dharura
Viongozi wa kiarabu na kiislamu wakiwasili Doha, Qatar kwa mkutano wa dharura. Picha: Qatar News Agency/REUTERS

Mwito huo umetolewa kupitia tamko la pamoja la viongozi wa karibu mataifa 60 wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ile ya nchi za kiislamu baada ya kumalizika kwa mkutano wao wa dharura uliofanyika jana mjini Doha.

Viongozi hao wamesema mbali ya kutafakari upya mahusiano ya kidiplomasia na Israel, mataifa yote wanachama yanapaswa kuchukua hatua za kisheria na kiutendaji kuizuia Israel kuendelea na hujuma dhidi ya Wapalestina.

Mashambulizi ya Israel ya mjini Doha yamelemaza juhudi za kidiplomasia zilizokuwa zikiongozwa na Qatar na Misri kujaribu kumaliza vita vya karibu miaka miwili kwenye Ukanda wa Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW