1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za Magharibi zahimiza utulivu baada ya uchaguzi Kongo

Hawa Bihoga
24 Desemba 2023

Mabalozi wa nchi za Magharibi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamehimiza utulivu baada ya viongozi wa upinzani kuutaja uchaguzi wa juma hili kuwa ni wa "kutoaminika" na wengine wakitaka urudiwe.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | Mpiga kura akihakiki jina katika kituo cha kupiga kura Kanyaruchinya.
Mpiga kura akihakiki jina lake katika orodha ya wapiga kura nje ya kituo cha Kanyaruchinya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: THOMAS MUKOYA/REUTERS

Hatua hiyo inatokea baada ya viongozi watano kutoka vyama vya upinzani nchini humo katika taarifa yao ya pamoja kuitisha maandamano siku ya Jumatano.

Balozi 12 ya mataifa ya Ulaya na Ubalozi wa Kanada katika taarifa ya pamoja wametoa wito kwa Wakongomani kuwa watulivu wakati huu ambapo zoezi la kuhesabu kura bado linaendelea.

Soma pia:Wagombea wa upinzani Kongo wanapanga maandamano ya kupinga uchaguzi wa rais

Takriban watu milioni 44 katika taifa hilo lenye watu milioni 100 walijiandikisha kupiga kura, huku zaidi ya wagombea 100,000 wakiwania nyadhifa mbalimbali. Rais Felix Tshisekedi anagombea muhula wake wa pili dhidi ya wagombea wengine 18 wa upinzani.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW