Nchi za Mashariki mwa Afrika zaongoza kwa maambukizi HIV
22 Julai 2024Takwimu kutoka mwaka 2023 zinaonesha maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha ugonjwa huo, na vifo vimepunguwa na kumeshuhudiwa hali iliyoimarika ya upatikanaji wa tiba kwa wagonjwa.
Hata hivyo shirika la kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa, UNAIDS limetahadharisha kwamba hatua zilizopigwa bado ni dhaifu. Mkuu wa shirika hilo Winnie Byanyima akizungumza mjini Munich kunakofanyika mkutano wa kimataifa kuhusu kupambana na Ukimwi, amesema bado ulimwengu umebakia nyuma kuelekea malengo ya 2030.
Soma pia:WHO yathibitisha kisa cha maambukizi ya mafua ya ndege kwa binadamu India
Mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika yametajwa kuendelea kuwa maeneo yenye maakumbukizi zaidi. Watu milioni 20.8 wanaishi na HIV na 450,000 waliambukizwa mwaka jana.
Lakini pia kanda hiyo inatajwa kuwa moja ya maeneo yaliyopata mafanikio makubwa ya kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 59 tangu mwaka 2010.