1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za msitu wa Amazon zakutana juu ya ulinzi wa eneo hilo

8 Agosti 2023

Viongozi wa nchi nane za eneo la msitu wa Amazon wanakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14, wakiwa na mipango ya kufikia makubaliano juu ya masuala ya kupambana na ukataji miti.

Amazon
Msitu wa mvua wa AmazonPicha: cc-by-sa-2.5/Phil P Harris

Viongozi wa nchi nane za eneo la msitu wa Amazon wanakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14, wakiwa  na mipango ya kufikia makubaliano juu ya masuala ya  kupambana na ukataji miti na ufadhili wa maendeleo endelevu.

Viongozi kwenye mkutano huo wa kilele wa Shirika la Mkataba wa Ushirikiano wa Amazon (ACTO), unaofanyika katika mji wa Brazil wa Belem, wanaweza kukubaliana juu ya mkataba wa kukomesha ukataji miti hadi ufikapo mwaka wa  2030, pamoja na kukomesha uchimbaji haramu wa dhahabu. Pia wanaweza kukubaliana kushirikiana katika ulinzi wa mipaka ili kuzuia uhalifu wa mazingira.

Viongozi hao wanatarajiwa kutoa tamko juu ya makubaliano waliyofikia baadae leo. Mwenyeji wa mkutano, rais Lula da Silva aliahidi wakati wa  kampeni za uchaguzi kuitisha mkutano huo katika juhudi zake za kurejesha uongozi wa Brazil katika kulinda mazingira, baada ya kuongezeka kwa ukataji wa miti, wakati wa utawala wa rais Brazil wa hapo awali, Jair Bolsonaro.