1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Kamati ya siri Ethiopia yadaiwa kuamuru mauaji ya waasi

28 Februari 2024

Uchunguzi wa Shirika la habari la Reuters umeonesha, kamati ya maafisa waaandamizi katika jimbo la Oromiya lilitoa amri ya kufanyika mauaji ya kiholela na kamatakamata ili kusambaritisha uasi nchini Ethiopia.

Wanamgambo wa Ethiopia washambulia barabara ya Addis - Hawassa
Mashambulizi ya waasi yaliiweka Ethiopia katika hali ngumu.Picha: Shewangizaw Wegayehu/DW

Reuters ilifanya mahojiano na zaidi ya maafisa 30 wa serikali kuu na wale wa mitaa, majaji, wanasheria na waathiriwa wa dhuluma hizo zinazodaiwa kufanywa na mamlaka. Shirika hilo pia lilipitia nyaraka zilizoandaliwa na  wamasiasa wa eneo hilo pamoja na mamlaka ya mahakama.

Mahojiano haya na nyaraka hizo kwa mara ya kwanza zinaangazia utendakazi wa Koree Nageenyaa, Kamati ya Usalama yakiwa katika lugha ya Kioromo, ambayo ilianza kufanya kazi miezi kadhaa baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuingia mamlakani 2018. Hata hivyo uwepo wa kamati hiyo haujaripotiwa hapo awali.

Kamati ya usalama ilianza kazi baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuingia madrakani.Picha: AP/picture alliance

Maafisa watano wa sasa na wa zamani wa serikali waliambia Reuters kwamba kamati ndio kiini cha juhudi za Abiy kumaliza uasi wa miaka mingi wa Jeshi la Ukombozi la Oromo (OLA), ambalo linaashinikiza kujitawala kwa watu wa Oromo na zaidi haki za lugha na asili katika maeneo hayo.

Soma pia: Abiy Ahmed akanusha watu kufa kwa njaa Ethiopia

Waoromo wamelalamika kwa muda mrefu kutengwa kisiasa na kijamii. Na pale ambapo maandamano ya mwaka 2019 yalipozuka serikali ilichukua hatua kali dhidi ya jamii hiyo, ambapo maafisa hao watano waliongeza kusema operesheni hiyo iliongozwa na Koree Nageenyaa.

Vurugu za eneo la Oromiya zimesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao. Serikali ya Ethiopia na maafisa wa haki za binadamu walilitupia lawama kundi la OLA kwa kuua raia wengi tangu 2019, tuhuma ambazo hata hivyo kundi hilo limezikanusha.

Madhila ya njaa Tigray baada ya vita

01:30

This browser does not support the video element.

Mmoja kati ya vyanzo hivyo wa Reuters alikuwa huru kutambulishwa jina lake, Milkessa Gemechu. Wengine, ikiwa ni pamoja na watu wawili ambao walihudhuria mikutano ya Koree Nageenyaa, waalizungumza katika masharti ya kutotaka kufahamika. Watu wanaofahamu kazi za Koree Nageenyaa ni kwamba inahusishwa na mauaji ya idadi kadhaa ya watu na na wengine mamia kutia mbaroni.

Miongoni mwa mauaji hayo, watoa taarifa walisema ni pamoja na yale mauwaji ya wachungaji 14huko Oromiya ya 2021 ambayo serikali hapo awali alilibebesha mzigo kundi la OLA.

Reuters iliwasilisha matokeo ya uchunguzi wake kwa mkuu wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia (EHRC) iliyoteuliwa na serikali, Daniel Bekele. Na baada ya kuhiojiwa, Bekele alithibitisha kuwepo kwa

Koree Nageenyaa, akisema lengo lake ni kushughulikia changamoto za kiusalama katika eneo la Oromiya, lakini ingawa ilipitiliza mipaka yake hadi hatua ya ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Ethiopia yatangaza hali ya hatari

01:20

This browser does not support the video element.

Bila ya kutoa ufafanuzi wa kina Bakele alisema "Tuna rekodi za visa vingi vya  mauaji ya holela, kuwekwa kizuizini kiholela, mateso na unyang'anyi."

Serikali ya shirikisho ya Ethiopia, ofisi ya Waziri Mkuu Abiy na serikali ya mkoa wa Oromiya haikujibu kwa kina maswali kuhusu uchunguzi huo wa Reuters. Huko nyuma Abiy amewahi kuitetea rekodi ya serikali ya kwa suala la haki za binadamu. Itakumbukwa tu, Februari 6, aliambia bunge wakati wa maswali ya kawaida: "Kwa kuwa tunafikiria katika misingi ya kidemokrasia, ni ngumu kwetu hata kumkamata mtu yeyote kiholela."

Soma pia: Abiy Ahmed atangaza uwezekano wa mazungumzo na waasi wa Oromo

Machafuko katika maeneo ya Oromiya, mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, ni ukumbusho wa kuendelea kukosekana kwa utulivu katika eneo zima la Pembe ya Taifa la Afrika. Ethiopia ipo katika mkondo wa kuvurugwa kwa migogoro. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miwili kaskazini kabisa mkoa, Tigray, iliua mamia ya maelfu ya watu hadi makubaliano ya amani yaliafikiwa mnamo Novemba 2022.

Mapigano yalizuka mara ya mwisho Julai katika eneo jingine la kaskazini la Amhara, kati ya jeshi la Ethiopia na wanamgambo. Kwa wakati huo serikali ililaizimikaa kutangaza hali ya hatari.

Abiy Ahmed ashinda tuzo ya Amani ya Nobel 2019

01:41

This browser does not support the video element.

RTR

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW