1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSierra Leone

Rais wa zamani wa Sierra Leone ashtakiwa kwa uhaini

4 Januari 2024

Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, amefika mbele ya mahakama kujibu mashtaka ya uhaini wa kiwango cha juu.

Rais wa zamani wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ashtakiwa kwa uhaini
Pichani ni Rais wa zamani wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa usuluhishi wa mzozo wa uchaguzi nchini Gambia Disemba 13, 2016Picha: Afolabi Sotunde/REUTERS

Rais huyo Ernest Bai Koroma anadaiwa kujihusisha na kile ambacho serikali ilikiita jaribio la mapinduzi la mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka uliopita.

Koroma aliyekuwa rais kati ya mwaka 2007 na 2018 alihojiwa na polisi mara tatu kabla ya kufunguliwa mashtaka.

Anahusishwa na mashambulizi ya silaha katika kambi kubwa ya jeshi nchini humo pamoja na gereza lenye ulinzi mkali lililopo kwenye mji mkuu, Freetown Novemba 26.

Karibu wafungwa 2,000 walitoroka katika shambulizi hilo, miongoni mwao wakiwa ni watuhumiwa waliohusishwa na mapinduzi hayo. 

Zaidi ya watu 50 wamekamatwa wakihusishwa na mashambulizi hayo, ikiwa ni pamoja na binti wa Koroma.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW