1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchini Syria hakuna ushahidi wa kufichwa silaha za Iraq

15 Novemba 2003

WASHINGTON: Marekani haina ushahidi wowote wa kuweko silaha za kuangamiza za Kiiraq katika nchi jirani Syria, alisema Mshauri wa Mambo ya Usalama wa Kimarekani Bibi Condoellezza Rice. Japokuwa amesoma ripoti, lakini hadi sasa hakuna ushahidi wowote unaoweza kuthibitisha shutuma hizo, Bibi Rice aliliambia shirika moja la utangazaji la Kimarekani mkoani Florida. Mabingwa wa silaha wa Kimarekani nchini Iraq wamekuwa wakifanya taftishi kuchunguza iwapo silaha marufuku au zana za kuundia silaha marufuku zilihamishwa kutoka Iraq na kupelekwa Syria au Jordan. Syria imewekwa katika orodha ya nchi zinazoshutumiwa na Marekani kuwasaidia magaidi. Pia Marekani inaishutumu Syria kuwa na niya ya kuunda silaha za kuangamiza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW