1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege isiyo na rubani ya Italia yadunguliwa Libya

21 Novemba 2019

Vikosi tiifu kwa mbabe wa kivita Khalifa haftar nchini Libya vimesema vimedungua ndege isiyo na rubani ya Italia, magharibi mwa Libya, iliyokuwa ikiruka katika eneo la anga wanalolidhibiti.

Drohne mit Kamera
Picha: picture-alliance/CHROMORANGE/C. Suhrbier

Wizara ya ulinzi ya Italia imesema kwamba ndege hiyo isiyo na rubani ilianguka katika eneo la Libya wakati ikifanya kazi ya kuhakikisha usalama wa machimbo ya mafuta pamoja na wavuvi wa Libya.

Hayo yanajiri siku kadhaa baada ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya kuzitaka nchi za kigeni kuheshimu vikwazo vya kuingiza silaha.

Libya imetumbukia katika machafuko tangu vuguvugu lililoungwa mkono na jumuiya ya kujihami NATO kumuondoa madarakani na kumuua kiongozi wa muda mrefu Moamer Kadhafi mwaka 2011.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW