1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ya abiria ya Cyprus imeanguka

14 Agosti 2005

Athens:

Ndege ya Cyprus ikiwa na Watu 121 imeanguka milimani leo kaskazini mwa Athens muda mfupi kabla ya kutua. Televisheni ya Kigiriki ya Alpha imetangaza kuwa Rubani amewaarifu wanaoongoza safari za ndege kuwa ndege hiyo ya aina ya Boeing 737 ilikuwa na matatizo ya kisafisha hewa . Muda mfupi baadaye mawasiliano yalikatika na ndege hiyo iliyokuwa inatoka Larnaca hadi Prague kupitia Athens. Polisi na Wazima moto walioko katika sehemu ajali ilipotokea wamesema kuwa hakuna aliye nusurika. Msemaji wa polisi wa Ugiriki amesema kuwa ndege ilikuwa na abiria 115 na Wafanyakazi sita. Watu wazima 59 na Watoto wanane walikuwa wakielekea Athens wakati ambapo abiria wengine 48 walikuwa wakielekea Prague.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW