Ndege ya Ethiopia yapata ajali ikielekea Nairobi
10 Machi 2019Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia imeanguka leo asubuhi majira ya saa mbili na dakika arobaini na nne kwa saa za Afrika Mashariki ikiwa na abiria 149 pamoja na wafanyakazi 8. Msemaji wa shirika hilo ambaye hakutowa jina lake amethibitisha juu ya taarifa hiyo ambapo imetajwa ndege hiyo ilikuwa ikielekea mjini Nairobi nchini Kenya. Waziri mkuu wa Ethiopia ameandika katika ukurasa wake wa Twitta leo Jumapili,10.03.2019 ujumbe wa kutoa pole kwa familia za waliofiwa kufuatia ajali hiyo mbaya.Ingawa pia ujumbe huo haukutowa maelezo zaidi.Ujumbe umesema-
''Ofisi ya waziri mkuu kwa niaba ya serikali na wananchi wa Ethiopia tungependa kutowa pole zetu kwa familia zilizopoiteza wapendwa wao waliokuwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikielekea Nairobi Kenya asubuhi ya leo''
Ndege hiyo ilikuwa ikitokea jijini Adis Ababa.
Mwandishi:Saumu Mwasimba
Mhariri:Sylvia Mwehozi