1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Ndege ya kivita ya Myanmar yaanguka wakati wa mapigano

12 Novemba 2023

Ndege ya kivita ya Myanmar imeanguka wakati wa mapigano makali kati ya jeshi na kundi la waasi. Hayo yameelezwa na pande zote mbili,katika kile kinachoonekana ni pigo jingine kwa utawala wa kijeshi wa Myanmar.

Waasi wa TNLA wa Myanmar
Waasi wa TNLA wa MyanmarPicha: AFP

Utawala huo unakabiliwa na upinzani mkubwa tangu ulipotwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka 2021.

Ndege hiyo ya kijeshi ilianguka katika jimbo la Kayah,mashariki mwa Myanmar karibu na nchi hiyo inakopakana na Thailand,jana Jumamosi. Jeshi linapambana na kundi la waasi la KNDF ambalo limedai kuidungua ndege hiyo.

Hata hivyo msemaji wa utawala huo wa kijeshi Zaw Min Tun,akizungumza kupitia kituo cha televisheni cha taifa, alidai ndege hiyo ilianguka kutokana na matatizo ya kiufundi.China imezitaka pande zote mbili kusitisha vita.